Friday

Hii ndiyo sababu ya Rais Magufuli kuvunja bodi ya TRA

4-7 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ametoa sababu iliyopelekea kuvunja Bodi ya Mamlaka ya Mapato (TRA ).
Rais Magufuli ameyasema hayo Alhamisi hii wakati akiongoza mahafali ya 31 ya chuo kikuu Huria yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.
“Juzi hapa tumekuta hela twenty six billion zilizokuwa zimetolewa TRA kwaajili ya matumizi ya TRA zikapelekwa kwenye mabenki matatu kama fixed diposit akaunti na bodi ikapitisha, ndio maana nilipozipata hizo hela nimezichukua na bodi kwaheri,” alisema.
“Kumekuwa na mchezo huu kwa machief excutive wengi zinapotolewa fedha kwaajili ya kwenda kwenye miradi fulani zile fedha wale machief executive wanazichukua wanaziweka kwenye commecial bank, wanaweka kwenye fixed diposit akaunti kwa mazungumzo ya uelewano kati ya huyo mkuu wa taasisi na mabenki husika. Waziri hiyo message sent and delivered,” alisisitiza.
Rais Magufuli alitengua bodi hiyo iliyokuwa chini ya mwenyekiti wake, Benard Mchomvu Novemba 20 mwaka huu.

SHARE THIS

0 maoni: