Shirika la umeme nchini TANESCO limesema halina mpango wa kupandisha bei
za umeme kwa watumiaji wadogo na badala yake mpango huo upo kwa
watumiaji wakubwa.
“Niwatoe hofu wananchi kwamba yale mapendekezo tuliyoyapeleka wananchi wa kawaida wale wanaotumia umeme mdogo bei zao hazitaathirika sana. Kuna jambo moja ambalo tumelitazama kwa mtazamo tofauti, unajua sasa hivi we mteja wa kawaida unalipa sawasawa na kampuni zinazoweka mabango barabarani ambazo ni kampuni za kibiashara,” alisema Mramba.
“Sasa katika mapendekezo tuliyopeleka EWURA tulikuwa tunamuomba aangalie kwamba yale makampuni yanayofanya biashara za mabango ya matangazo yasilipe sawasawa na mteja wa nyumbani bei yake iende juu zaidi.”
0 maoni: