Baada ya msanii Nay wa Mitego kuachia
wimbo wake wa shika Adabu Yako yamesemwa mengi katika mtandao ya
kijamii, kutokana na msanii huyo kutumia kipaji chake kuwachana mastaa
mbalimbali hapa Bongo akiwemo Shilole, Snura, Wema Sepetu, Ray, Niva,
Shetta na wengine wengi.
Katika hao mastaa aliowataja kwa majina
kwenye ngoma yake wapo walioibuka na kujibu tuhuma kwa njia mbalimbali
ikiwemo kupitia vyombo vya habari au kurasa zao za Instagram, huku
wakionesha kuto pendezeshwa na kitendo cha msanii huyo kuwachana na
kuwafanya waonekane tofauti mbaele ya jamii inayo wazunguka.
Kwa upande wake mmoja wa wasanii ambao
wametajwa katika ngoma hiyo Shetta hitmaker wa Shikorobo, amekuwa na
mtazamo tofauti kuhusu nyimbo na video ingawa katika nyimbo hiyo
ametajwa kununuliwa gari na tajiri mmoja ambaye ni mdau wa burudani
maarufu kama Chief Kiumbe, na katika video hiyo anaonekana mwanaume
aliyeigiza kama Shetta akishikwa makalio jambo ambalo limezua mjadala na
mitazamo tofauti.
Shetta amefungukia suala hilo katika
mahojiano yake na kipindi cha Planet Bongo cha East Afrika Radio na
kueleza kuwa Nay ni rafiki yake wa muda mrefu hivyo hawana tatizo lolote
na kilichooneshwa kwenye video ya shika Adabu Yako kwake ni kichekesho,
huku akisisitiza kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa gari na anazo
nyaraka zote kuthibitisha hilo, huku akieeleza kuwa huenda Nay hakujua
kuhusu gari lake ndio maana akaamua kuimba hivyo.
0 maoni: