Hivi karibuni kumeibuka mengi kumuhusu
msanii Baraka Da Prince ikiwemo kuhusishwa kutoka kimapenzi na mastaa wa
bongo akiwemo Menina na muigizaji mahiri nchini anae tamba na filamu
yake ya Kiboko Kabisa Salima Jabu maarufu kama Nisha, vile vile Baraka
Da Prince anahusishwa na skendo ya kumpatia ujauzito mwanadada kutoka
Iringa anaefahamika kwa jina la Farida.
Baraka Da Prince amekuwa akihojiwa mara
kadhaa na vituo mbalimbali vya habari kuhusu suala hilo ambapo amekuwa
akikanusha na kueleza kuwa hajawahi kutoka na staa yeyote, hivyo habari
zinazo sambaa kuhusu yeye hazina ukweli wowote.
Katika pitapita ya mtembezi mitandaoni
imekutana na post ya Baraka Da Prince akieleza masikitiko yake kutokana
na kuhusishwa na mambo ambayo siyo ya kweli huku akisema ni njama za
kumuharibia kisanaa, vile vile kwenye post hiyo Baraka amemuanika mpenzi
wake na kueleza kuwa huyo ndiye anae mtambua hao wengine hawatambui.
0 maoni: