Baada ya msanii Emanuel
Elibariki maarufu kama Nay Wa Mitego kuachia wimbo wake wa Shika Adabu
yako ambao amewachana mastaa mbalimbali akiwemo Wema Sepetu, Niva,
Snura, Shilole,Shetta, Ray na wengine wengi amejikuta akiingia katika
mitihani mikubwa ambapo hivi karibuni alikuwa anafuatiliwa na mtu kila
sehemu alipokuwa anakwenda.
Vilevile baada ya kutangaza
kuwa siku ya Ijumaa angeachia Video yake akiwa njiani akavunjiwa kioo
cha gari lake ,hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza mkasa
mzima na kusisitiza kuwa hatoacha kusema ukweli kwa kufanya kile
anachoona ni sahihi kwake.
“Nimevunjiwa kioo Cha gari nikiwa njiani naenda kwenye Interview Chanel5 EaTv kwa ajili ya kutambulisha my New Video #ShikaAdabuYako sorry
Watu wangu mliokua mkisubiri kuona Video Na Interview yote nimeshindwa
kufika naweka sawa ili. Video itaenda YouTube kesho itakua kwenye Tv
yako Pendwa. Muziki sio vita. I will never stop doing what i do.!! ”
ameandika Nay Wa Mitego kupitia ukurasa wake wa Instagram
0 maoni: