Thursday

Rufaa ya Trump kurudisha marufuku ya waislamu kuingia US yapigwa chini, sasa ruksa

Mahakama ya rufaa nchini Marekani imelikataa jaribio la Rais wa nchi hiyo, Donald Trump kurejesha amri yake ya kuzuia wageni kutoka nchi saba za kiislamu kuingia nchini humo.
Mahakama hiyo imesema haitoweza kuzuia agizo lilitolewa na mahakama ya chini yake. Trump aliujibu uamuzi huo kwa hasira kwenye Twitter akidai usalama wa nchi upo matatani.
Majaji watatu kwenye mahakama hiyo wamekubaliana pamoja wakidai kuwa serikali haijatoa uthibitisho wa uwepo wa tishio la kigaidi kuhalalisha marufuku hiyo. Uamuzi huo una maanisha kuwa watu kutoka Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen walio na visa wanaweza kuingia Marekani.
Na wakimbizi kutoka duniani kote waliokuwa wameathirika na marufuku hiyo nao hawatazuiwa tena.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwenye mahakama kuu.

SHARE THIS

0 maoni: