Saturday

Dkt Shein aongeza mshahara kwa asilimia 100

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ametangaza neema mpya kwa wafanyakazi visiwani humo baada ya kuwahakikishia kupandisha kima cha chini cha mshahara kuanzia mwaka huu .
Dkt. Shein ameyasema hayo wakati akiwaongoza watanzania kuadhimisha Miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Amani visiwani humo.
“Niliahidi kutekeleza ahadi hii ya kiwango cha mshahara kwa kima cha chini mshahara utaongezeka kutoka shilingi 150,000 hadi shilingi 300,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100, ingawa nitapata ridhaa tena ya kuongoza nchi katika kipindi changu cha pili, ninaahidi nitatekeleza tena katika mwaka wa fedha ujao,” alisema Dkt Shein.
Katika hatua nyingine Dkt Shein alizungumzia jinsi anavyodhibiti matumizi ya fedha ya siyo ya lazima katika serikali yake ” Jitihada za kudhibiti matumizi zilizochukuliwa na serikali zimefanikiwa, serikali itaendelea kuyadhibiti matumizi ambayo siyo ya lazima na kwamba fedha za serikali zitaendelea kuwahudumia wananchi kwa mambo muhimu kwa maendeleo yao”.

SHARE THIS

0 maoni: