Saturday

Tanesco kuuanza mwaka mpya na bei juu za umeme

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (EWURA) imetangaza ongezeko la bei ya umeme kwa wastani wa asilimi 8.5.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta ‘EWURA’ Felix Ngamlagosi.
Akizungumza Ijumaa hii na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta ‘EWURA’ Felix Ngamlagosi alisema baada ya EWURA kufanya uchambuzi wake haikuona sababu ya kuongeza kwa asilimia 18.19 badala yake ikapunguza hadi wastani wa asilimia 8.5.
“Pendekezo lao lilikuwa linalenga kuongeza bei ya umeme kutoka wastani wa shilingi 242.2 kwa uniti hadi shilingi 286 kwa uniti, sasa tumepunguza katika makundi yote ya wateja, na tumekataa kuongeza gharama ya asilimia 5 kwenye kundi la watumiaji wa uniti chini ya 75 kwa mwezi,” alisema Ngamlagosi.
Aidha katika hatua nyingine alisema kuwa masharti walioyatoa katika shirika hilo ni pamoja na kuongeza huduma katika kundi la D1 linalogusa watumiaji wa chini ya uniti 75 kwa mwezi. Oktoba 4 mwaka huu shirika la umeme Tanzania(TANESCO) liliwasilisha ombi la kupandisha gharama za umeme kwa mamlaka hiyo.

SHARE THIS

0 maoni: