Monday

Lukuvi aagiza wamiliki ardhi kupewa hati

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ameagiza kwa wananchi wote wanaomiliki viwanja vya makazi kuhakikisha wanachukua hati za umiliki ifikapo Machi 30, mwakani.

lukuvi-photo1

Ametoa agizo hayo mwishoni mwa wiki akiwa mkoani Shinyanga wakati alipofanya ziara katika wilayani Kishapu, ambapo alikuwa na kazi kubwa ya kutatua kero za wananchi katika sekta ya ardhi huku akisisitiza viongozi wa sekta hiyo kutatua changamoto hizo haraka.
Lukuvi alisema serikali imedhamiria kutatua kero za ardhi na ina mkakati wa kuwasaidia wananchi wawe na hati halali za viwanja wanavyomiliki huku akiwaahidi kupata hati zao ndani ya mwezi mmoja kwa atakayelipia mapema.
Aidha Lukuvi alisema kuwa suala la hati ni la lazima na kuwa inamsaidia mwananchi kuwa na usalama na kiwanja chake na kupata huduma mbalimbali kama mikopo ya benki.
Hivi karibuni waziri huyo atoa mwezi 1 kwa viongozi wa serikali ngazi za kijiji hadi mkoa kutatua migogoro ya ardhi.

SHARE THIS

0 maoni: