Walter Chilambo aanza kufanya muziki wa gospel
Mshindi wa shindano la kusaka vipaji la BSS 2012, Walter Chilambo amezungumzia maisha yake mapya ndani ya muziki wa gospel baada ya kuutosa muziki wa bongofleva.
Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Chilambo amesema ameamua kuamia upande wa muziki wa gospel ili kufanya kile anachokipenda.
“Kwa sasa mimi nitakuwa namuimbia Mungu, hata wimbo wangu mpya ‘Asante’ namuimbia Mungu, ni wimbo wa gospel na nimeamua kumshukuru mwenyezi mungu kwa sababu tunapitia mambo mengi sana sisi kama vijana. Kwa hiyo nimekaa na familia na mimi mwenyewe nikaona nifanye kitu ambacho moyo wangu utakuwa unafurahia pia naimani hata jamii nayo itakuwa rahisi kunisupport kwahiyo najaribu huku labda Mungu ana mpango na mimi,” alisema Walter.
“Kwenye bongofleva sidhani kama wataniona tena sijui kitokee kitu gani lakini nitakuwa nafanya muziki wa mungu na mambo mengine yakijamii lakisi sio kwenye muziki wa bongofleva. Ni muda mrefu sana nilikuwa natamani kufanya hiki kitu na hawawezi kuniamini kwa sababu hawakunisikia mahali popote, wamekuja kunisikia kwenye muziki wa bongofleva tu lakini hata ukiniangalia kwenye mashindano ya BSS mimi sikuwa mtu wa fujo fujo, sikuwa mtu wa ajabu ajabu wala sikuwa mtu wa skendo,” aliongeza Chilambo.
0 maoni: