Siku chache zilizopita, kulitokea sintofahamu baada ya Wizkid
kutangazwa mshindi ilhali kwenye website ya tuzo hizo, kura zilionesha
kuwa ni Alikiba ndiye aliyeshinda.
Alikiba amethibitisha taarifa hizo wakati akichat live Jumatano hii kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Amesema baada ya mashabiki wake kulalamika kuhusiana na mkanganyiko
huo, MTV EMA walifuatilia na kukiri kuwa na makosa na kuutumia ujumbe
uongozi wake kuwa Alikiba ndiye mshindi halali, na sio Wizkid.
“Sasa ndio nimepata confirmation kwamba ni kweli tuzo inakuja
Tanzania na vile vile mimi siwezi kuzungumzia, nitasubiri mpaka
nizishike,” amesema Kiba.
Muimbaji huyo amedai kuwa habari hizo amezipokea kwa furaha kubwa na
kuwashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha kushinda na kuwa nyuma yake.
Wakati hup huo Kiba amempongeza Wizkid kwa ushindi wa tuzo nyingine
ya Afrima. Kwa upande wa Wizkid, tayari amefuta post zote za Instagram
alizokuwa ameweka kushangilia ushindi huo.
0 maoni: