Shilole amempongeza Nuh Mziwanda kwa kuongeza idadi ya wasanii
walioukimbia ukapera baada ya kufunga ndoa kimya kimya na mpenzi wake
Nawal.
Kupitia mtandao wa Instagram, Shilole ameandika ujumbe unaosomeka,
“Hongera Nuh Mwenyezi Mungu awatie baraka tele kwenye ndoa yenu.”
Hitmaker huyo ameungana na mastaa wengine waliofunga ndoa mwaka huu
akiwemo Mwana FA, Shamsa Ford, Nyandu Tozzy, Tunda Man, Mabeste na
wengine.
Nuh na Shilole waliwahi kuwa wapenzi kwa muda mrefu lakini mwishoni
mwa mwaka jana waliachana huku kila mmoja akianzisha mahusiano mapya.
0 maoni: