Monday

NICK WA PILI AWATETEA MTV EMA, WALIKOSA UMAKINI TU NAO NI WATU


Nick wa Pili amesema kosa lililofanywa na MTV EMA, kumtangaza mshindi wa Best Africa Act Wizkid na kisha kuja kumpa Alikiba aliyepata kura nyingi, ni la kibinadamu na kwamba wanapaswa kuwa makini tu.
“Mi naona walikosa umakini, lakini kukosea ni kitu cha kawaida, as long as waligundua wamekosea na wakafanya kitu sahihi sio kama kuna tatizo,” Nick alimwambia mtangazaji wa kipindi cha The Vibe cha Mashujaa FM ya Lindi, Baby Dinny.
Nick amedai kuwa kosa walilolifanya limeonesha kuwa wao ambao wanatazamiwa kuwa na umakini wa hali ya juu nao hukosea.

SHARE THIS

0 maoni: