Saturday

BASATA: BIFU YA DIAMOND NA ALIKIBA TUKILETEWA KIOFISI TUTAIMALIZA

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) ambalo ni walezi wa wasanii pamoja shughuli za sanaa nchini, limekiri kusikia tetesi ya bifu inayoendelea kati ya mastaa wawili wa muziki nchini, Alikiba na Diamond.

Akizungumza naKwetu Flaver wiki hii, Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amesema amesikia kuna bifu kati ya Diamond na Alikiba lakini hawajapokea taarifa rasmi ambayo inayoonyesha mmoja kati yao akilalamika kuhusu mwenzie.
“Kwa upande wa serikali au BASATA tunafanya kazi kwa kuzingatia maandishi au taarifa rasmi, kwahiyo suala (la Alikiba na Diamond) halijatufikia rasmi,” alisema Mngereza. “Huu ni ushabiki au mashabiki ndio wanaleta haya, kwa hiyo ni ushabiki wa team hii na hii na tunaliona. Lakini kwa kuwa halijaja rasmi likija rasmi tutalishughulikia,”
Aliongeza, “Lakini tukikutana na wao wenyewe wapo safi, kwa hiyo wanaosababisha hivyo ni mashabiki kwa sababu hata wachezaji wa Simba na Yanga wale ni wachezaji wapo kwenye tasnia moja, ni marafiki wanakaa pamoja, wanakula pamoja ni kama wanamichezo wa ngumi, wewe ukiwa nje unaangalia wao wanapigana kweli lakini ule ni mchezo. Kwahiyo mimi hii naona ni ushabiki wa mashabiki ambapo kimsingi huwezi kuwazua. Pia ni kwa sababu hakuna aliyelalamika, kimsingi sisi ni walezi wa wasanii mmoja angelalamika sisi tungeuwita upande mwingine,”


SHARE THIS

0 maoni: