Tuesday

Alikiba aicheka kauli ya Diamond kuhusu pete ya kijani!

Je unaikumbuka kauli ya Diamond aliyoitoa wiki iliyopita kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM kuhusu pete ya kijani?
 
15056662_331170897262349_6840282975670632448_n
Ngoja nikukumbushe japo kidogo kile alichokisema, “Mimi sina matatizo na watu ndio maana wakijaribu kushindana na mimi huwa wanashindwa. Hata ukiniangalia sina hata pete ya kijani kwenye vidole vyangu.”
Kumbe alikuwa amerusha jiwe gizani kwa upande wa pili. Inawezekana Alikiba ameshtuka hilo kutokana na picha aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram na kuandika, “Pete Ya Kijani
#BirthdayLoading29thNoV #KingKiba.”

15101765_1872147946350780_2002734140499165184_n
Mwanzo ilionekana ilikuwa ni vita baridi ya maneno ya chini kwa chini kati ya mafahari hao lakini kwa sasa hakuna kilichojificha tena na kila kitu kipo wazi.
Wiki iliyopita hitmaker huyo wa Salome na Ommy Dimpoz walichafua hali ya hewa kwenye mtandao huo kwa kutupiana vita ya maneno ya kejeli na kukashifiana.

SHARE THIS

0 maoni: