Siku chache zilizopita, kulitokea sintofahamu baada ya Wizkid kutangazwa mshindi ilhali kwenye website ya tuzo hizo, kura zilionesha kuwa ni Alikiba ndiye aliyeshinda.
Lakini baada ya MTV EMA kujua makosa yao, waliamua kumpokonya tuzo ya Best African Act na Worldwide Act, Wizkid na kumpa Alikiba ambaye alistahili kushinda.
Baada ya taarifa rasmi ya MTV EMA, Alikiba ameandika:
Namshukuru MUNGU Na Shukrani kwa MTV kwa heshima hii, nina furaha sana kwa ushindi huu, ni heshima kwangu na nchi yangu Tanzania pamoja na East Africa nzima kiujumla. Shukrani sana kwa familia yangu, management yangu na mashabiki zangu wote – nawapenda sana #bloodfanswaalikiba #Kajiandae #KingKibaAliongeza,
“Ningependa pia kuchukua nafasi hii kushukuru vyombo vya habari vyote, watangazaji, waandishi na wadau wote wa sanaa kiujumla kwa kunisapoti katika kazi zangu. Lastly, nawashukuru wasanii wenzangu wote mlionipa ushirikiano na kuthamini kipaji changu kwa kuniombea kura zilizonipa ushindi. Ushindi wangu ni ushindi wa sanaa yetu sote. Proudly Tanzanian MUNGU awabariki sana. #TupoPamoja #Kajiandae #KingKiba
Namshukuru MUNGU Na Shukrani kwa MTV kwa heshima hii, nina furaha sana kwa ushindi huu, ni heshima kwangu na nchi yangu Tanzania pamoja na East Africa nzima kiujumla. Shukrani sana kwa familia yangu, management yangu na mashabiki zangu wote – nawapenda sana#bloodfanswaalikiba #Kajiandae#KingKiba”
0 maoni: