Hiki ndicho alichoiandika Mr Muleba katika acount yake ya instagram baada ya kuwa na hofu na soka la bongo kutopewa kipau mbele huku wachezaji wa nchi za nje wakinunuliwa kwa mabilioni wakati wabongo wenye viwango kuzidi wachezaji na nchi za nje wakinunuliwa kwa bei ya kudhararuliwa.
"
Soka,Kabumbu,kandanda ni maneno yenye mvuto kwenye vinywa vya
wapenda mchezo huo.lakini mengi zaidi ni pale mchezo huo wenye
mashabiki wengi duniani unapokosa nguvu ktk Taifa letu lenye kila kitu
Tanzania.Tim ya taifa haifanyi vizuri pamoja na club zetu
vilevile.shirika lipo linahusika katika masuala mazima ya kulipandisha
na kulishusha soka la Tanzania.T.F.F wanaona na kubariki kila
kinachoendelea kwenye mchezo huu.watanzania tunapenda mchezo huu ila
ndo hivyo zengwe kila kona.hainiingii kichwani pale unapoona mchezaji
anatoka Brazili ananunuliwa kwa mamilioni ya mamia ya fedha na hali
pale temeke yupo kijana anaepatikana kwa bei ya dharau na mwenye uwezo
zaidi ya mbrazili huyo.Taifa linakosa hela ya maana kwa kutopata ukweli
wa bei halali ya biashara kati ya mchezaji husika na club T.F.F
wamelala.hainiingii akilini kuona mcheza mzawa wa taifa hili ambae
anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa wachezaji chipukizi anasajiliwa na
Tim kubwa kama Simba ama yanga usajili wa maigizo, mfano anaahidiwa
kitita cha tsh ml 10 anasainishwa mkataba anapewa m4 nyingine madeni
ambayo halipwi anaambulia chenga tu na baadhi ya viongozi mwisho wa
siku anaambulia vijiposho mshenzi na hali club inaendelea kusema uongo
kwa mashabiki juu ya bei husika kujionesha ina uwezo kwa kutangaza bei
ya manunuzi Mara mbili zaidi kitu kinachofanya mashabiki wampe majukum
mazito mchezaji wao kulingana na uongo wa viongozi.hatmae mchezaji
anapoteza morali ya kuwa ktk kiwango bora kutokana na matatizo kama
hayo.na hiyo michezo IPO ktk club kubwa tu.T.F.F mko wapi? Fanya
kujiuliza nani anafahamu ukweli wa bei za wachezaji wa club zao? Je
mnaficha nini hapo kati? Mchezo wa Mpira ni hela walipeni wachezaji
stahiki zao watupe burudani sahihi.undeni timu ya taifa kwa kuchunguza
vipaji vya wachezaji kwenye Tim zao zote kwa pamoja ondoa kukariri
kupata wachezaji kwenye Tim tatu tu.Tanzania itacheza mpira unaoandikwa
kwenye magazeti kuliko maigizo yalivyo kwa sasa yangu ni hayo kwa leo"
0 maoni: