Saturday

Mr Muleba Na Utetezi Juu Ya Original Comedy Kuvaa Sare Za Police


Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza  tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao za kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za Nchi. 
 

Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za makosa ya Jinai, sura ya 16 na  marejeo yake ya mwaka 2002,  kifungu cha 178 (1) na  (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama,  kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo  bila kibali kutoka kwa  Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia  kitendo kilichofanywa na kundi la kisanii la “ Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linachukua  hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.
 
Lakini leo utapata uchambuzi na utetezi kutoka kwa Mr Muleba ambaye anakuchambulia kwa kina zaidi kutokana na umuhimu wa wasanii hawa nchini kama wanahitaji kuelimishwa au serikali kuwajali endapo watahitaji hvyo vifaa vinapohitajika,Mr Muleba ameongeza kuwa anamuomba sana 'Mh.Waziri wa habari na michezo Ndugu Nape Nauye pamoja na Mh.waziri wa mamabo ya ndani Mh.Mwigulu nchembe awasaidie Original Comedy kwa tatizo hili na awajengee mazingira ya namna watakavyofanya wakihitaji kutumia vifaa vya kijeshi kama inaruhusiwa' Kayandika hayo katika acount yake ya instagram @Mr.muleba_only_one kama inavyoonekana hapo chini
 

Inasikitisha lakini hakuna namna kwakuwa kila kitu kinaenda kisheria na kilichobaki ni huruma juu ya watuhumiwa nakuangalia malengo yalikuwa yapi.Mh waziri tunakuomba uwasaidie vijana wako kuwanasua hapo waliponaswa.Tasnia ya comedy ni sehemu ya kuingizia nchi yetu kipato hivyo yapaswa kuangaliwa kwa jicho la pili na kuwakosoa pale wanapokosea.Na ikibidi wizara iwaombee kifungu cha kuwaruhusu wasanii wetu kwa pande zote kupata taratibu za kutumia sare za jeshi LA polisi ama vifaa na hata kufunga Barabara wakiwa kwenye shughuli yao ya kutengeza kazi husika ktk tukio husika.make kuna script zitakazo walazimu kuvaa kijeshi na awe na kifaru kwa mfano,kama kutakuwa na utaratibu wa kupata vibali na hatua za kuwalinda natumai tunaweza kupiga hatua na kufikia wenzetu walio tutangulia.Makosa ya sare za jeshi LA polisi na jeshi LA wananchi yanakuwa yanajirudia Mara kwa Mara juu ya kutumiwa na wasanii,kwanini iwe hivyo? Pengine kuna utaratibu wanaouruka waelimishwe kuhusu hilo ama serikali iwaandalie utaratibu mzuri wa kutumia na kupata vifaa pale watakapovihitaji.Nchi zinazoongoza katiba ubora wa tasnia ya filam miziki na comedy kama Marekani na India zinaonekana hata zikitumia majengo ya serikali.nini kinafanyika kwa wenzetu tukichunguze tuweze kukisogeza na hapa kwetu.Namaliza kwa kukupigia Goti Mh.Waziri wa habari na michezo Ndugu Nape Nauye pamoja na Mh.waziri wa mamabo ya ndani Mh.Mwigulu nchembe Wasaidie Original Comedy kwa tatizo hili na muwajengee mazingira ya namna watakavyofanya wakihitaji kutumia vifaa vya kijeshi kama inaruhusiwa.


SHARE THIS

0 maoni: