Friday

Mr Muleba Aelezea Jinsi Nguvu Ya Mwanamke Ilivomponza Baba Yake Mzazi Diamond Platnumz


Kutana na Kijana anayechambua kiundani maisha ya mtanzania ususani watu maarufu kama wasanii na viongozi wa nchi ambapo utaweza kuelewa sababu ya mtu kufeli au kufanikisha maisha leo kaja na hii soma alichoandika Mr Muleba kutoka katika acount yake ya Instagram @Mr.Muleba_only_one 


power.nguvu ya mwanamke ni nguvu ya aina yake waweza kusema ni nguvu ya kipekee.kwa kudhihirisha hilo nguvu ya mwanamke inaonekana pale ambapo Diamond platinum anamtelekeza baba yake mzee Abdul kwa ushawishi unaotokana na mama yake mzazi.mwanzoni mwa umaarufu wake inasadikika Diamond alikuwa karibu na baba yake japo haikuwa kiviiile.ajabu ubaya wa baba huyo kwa Diamond inaonekana unazidi kuongezeka kadri utajiri kwa mwanae unapozidi kuongezeka.upendo umepotea kadri mabilioni yanapozidi kutuna inasikitisha sana.hiyo yote ni nguvu ya mama.Maskini ya mungu Baba alimkimbia Mama kutokana na anayoyajua mwenyewe katika maisha yao na busara aliyoitumia nikutomuelezea mwanae nini kilichomkibiza toka kwa bibie hiyo yote ilikuwa nikumstiri lakini ikawa tofauti kwa mama alipotumia mwanya huo wa kumtbua mwenza wake kwa mwanae ili asipate msaada toka kwa bilionea huyo kijana.Diamond msamehe mzee wako ugomvi wa wazazi wako hukuujua hata wewe yaweza kukutokea na Tifah asijue ukarimu wako uufanyao kwake kwa sasa.Mama legeza kamba kwa mwenza wako yai lake lilikuwa na thamani kubwa kwako.haijalishi umrudishe kwenye himaya yako bali mrija wa mafanikio walau umdondoshee matone kwa umbali.tushakubali na kuiona Woman Power

Kama utapenda anachokifanya Mr Muleba waweza kumfollow insta @Mr.Muleba_Only_one


SHARE THIS

1 comment: