Friday

HARMONIZE: NAWEZA KUFANYA KAZI NA ALIKIBA


Harmonize wa AIYOLA ambaye hivi karibuni ameachia ngoma yake nyingine mpya na Diamond Platnumz (BADO) chini ya lebo ya WCB, ameweka wazi kuwa yuko tayari kufanya kazi ya kimuziki wakati wowote na Alikiba.

Katika mahojiano yake na kipindi cha Clouds360 cha Clouds  Tv, Harminze aliulizwa swali kama anaweza kufanya kazi na Alikiba.

Ambapo Harmonize aliesema licha ya msanii Alikiba, yupo tayari kufanya kazi na msanii yeyote hapa nchini ila kama ataiona mantiki ya kazi hiyo na kuridhika nayo. 

Hata hivyo Harmonize aliweka wazi kuwa hatoweza kuingia katika bifu la Diamond Platnumz na msanii mweingine isipokuwa kwa kupima uzito wa kosa

 


SHARE THIS

0 maoni: