Kufuatia kukithiri kwa wimbi la wasanii
wa nyumbani kufanya video zao nje ya nchi hususani Afrika Kusini na nje
ya hapo, rapa mwenye makeke kutoka nchini Kenya maarufu kama Prezzo
amewataka wasanii wa Afrika Mashariki kubadilika kimawazo na kuthamini
waongozaji wa ndani.
Akizungumzaia suala hilo katika kipindi
cha Clouds E kinacho rushwa na Clouds TV msanii huyo amesema wasanii
wamekuwa kama kondoo wakiona mmoja wao kafanya video nje nao wanaiga
wakiamini watafanikiwa, hivyo amewataka wasanii hao kufanya kazi na
waongozaji wa ndani kwani kuna sehemu nzuri (Locations), vitendea kazi
ambavyo vitaifanya kazi kuwa bora na kuwavutia wasanii wengine wa nje
kuja kuwekeza kwenye soko la ndani.
Prezzo yupo nchini kikazi akiambatana na
Menejimenti yake ambapo ameanza zoezi la upigaji picha wa video yake
mpya chini ya muongozaji anaekuja kwa kasi Afrika Mashariki kutoka
Wanene Film maarufu kama Hanscana.
vile vile msanii huyo ameweka bayana kuwa atafanya kolabo na baadhi ya wasanii wa Bongo akiwemo Mr Blue.
0 maoni: