Msanii mahiri kunako tasnia
ya muziki hapa nchini Q-Chila amesema haoni sababu yeyote ya kufanya
kazi na waongozaji wa nyumbani kwasababu hawana jipya na wameishakwama
kiubunifu .
Katika mahojino yake na moja
ya radio hapa nchini amesema ameshafanya kazi zaidi ya miaka 10 na
waongozaji wa ndani na haoni tena sababu ya kufanya nao kazi kwasababu
uwezo wao ni mdogo kuanzia ubunifu na hata vifaa vyao.
Q-Chief ameongeza kuwa waongozaji wadogo kama Hanscana na
wengine bado wanahitaji kujifunza zaidi lakini wamekuwa wakitoza pesa
nyingi jambo ambalo haoni kama wanafanya kazi yenye thamani ya kazi
hiyo.
Amefafanua zaidi na
kueleza kuwa unakuta Director anakuambia utoe milioni 17 wakati kiuwezo
ni mdogo kwahiyo ni bora akaenda kushoot nje kama wasanii wengine wa
bongo na atarudi kushoot na wa hapa pindi watakapo jifunza.
0 maoni: