Home »
HABARI
» Diamond Platnumz na Ne-Yo kufanyanyia Marekani na Afrika video ya collabo yao
Festo Baharia
Thursday, 29 October 2015
Diamond
Platnumz ambaye amefanya collabo na msanii mkubwa wa R&B wa
Marekani, Ne-Yo ameelezea hatua ilipofikia project hiyo inayotarajiwa
kumfungulia njia ya mafanikio zaidi kimataifa.
Akizungumza
na mtangazaji wa Citizen ya Kenya, Mzazi Willy Tuva, Platnumz amesema
kuwa wimbo huo umekamilika lakini hawezi kusema utatoka lini kwa sasa
kuna baadhi ya mambo ambayo anayoyaweka sawa kabla ya kuachia.
Diamond
ambaye wiki iliyopita aliibuka mshindi wa tuzo ya MTV EMA ‘Best
Worldwide Act Afrika/India’, amesema anafikiria kushoot video hiyo
nchini Marekani pamoja na Africa.
Ne-Yo
ambaye alikutana na kufanya kazi na Diamond wakati wa Coke Studio
Africa jijini Nairobi, Kenya alikuwa miongoni mwa mastaa waliompongeza
Baba Tiffah kwa ushindi wa MTV EMA kupitia Instagram kwa kuandika,
“CONGRATS TO MY HOMMIE @diamondplatnumz for winning #BestWorldWideAct at
the #MTVEMAs keep being great! Let’s go get em’ my guy!”
0 maoni: