Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kukusanya
jumla ya shilingi milioni 840 za faini ya makosa mbalimbali ya
barabarani kwa kipindi cha wiki moja ya oparesheni iliyofanywa na jeshi
hilo.
Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii, Kamishna wa Kanda Maalumu
ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kiwango cha mapato hayo ni kidogo
na inaashiria kupungua kwa makosa yanayofanywa na madereva.
“Kwa upande wa barabarani tunakwenda vizuri kati ya tarehe 1 mwezi 3
mwaka 2017 mpaka tarehe 9 mwezi wa 3 mwaka 2017 takribani siku hizo 8
tumeweza kukusanya jumla ya shilingi milioni 840 kwahiyo niseme tu
kwamba mapato yanapungua hii tu ni kwasababu watu wameanza kutii tu
sheria ya usalama barabarani,” Alisema Kamanda Sirro.
0 maoni: