MTUMISHI wa umma atakayeshindwa kuwasilisha cheti cha elimu na
taaluma au “Index number” ya mtihani ili zihakikiwe na Baraza la
Mitihani la Taifa (Necta), itakapofika Machi mosi mwaka huu, atakuwa
kajiondoa kazini mwenyewe, imeelezwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora), Angellah Kairuki alibainisha hayo mwishoni mwa wiki
wakati akifungua Mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
“Watendaji wakuu ninawaomba msimamie uhakiki wa vyeti ili watumishi
wenu wafanye kazi kwa sifa stahiki,” alisisitiza Kairuki, katika taarifa
iliyotolewa na wizara yake.
Aliongeza kwamba serikali ilisitisha ajira mpya ili kupisha kazi ya
kuondoa watumishi hewa, ambayo imefika ukingoni na siku za karibuni,
ajira zitarudishwa.
Akiwa mjini Dodoma, Septemba mwaka jana, wakati wa kuapishwa kwa
wakurugenzi watendaji wapya 13 walioteuliwa Septemba 10, mwaka huu,
Kairuki alisema kuanzia serikali imewaondoa watumishi hewa 17,201 kwenye
utumishi wa umma na kazi hiyo inaendelea.
Kairuki aliwataka watendaji wakuu kuweka mikakati ya kuepuka
watumishi hewa na kusimamia kwa dhati kwa sababu jambo hilo, limeumiza
na kupoteza rasilimalifedha nyingi za serikali.
Alisema anatambua kuna wakala zenye upungufu wa watumishi, hivyo
zinaingia gharama kubwa za kuajiri wafanyakazi wa mikataba, hata hivyo
alielekeza kila Mtendaji Mkuu ajiridhishe kwa kuandaa taarifa ya
mahitaji halisi ya watumishi.
Pamoja na hilo, Kairuki alielekeza wakala zenye watumishi wa mikataba
zifanye tathmini na kuhakiki kama kweli watumishi hao wanahitajika kwa
kuwa eneo hilo ni moja ya maeneo yenye ajira za mashaka kwa baadhi ya
taasisi.
Aliongeza kuwa yapo malalamiko kuhusu suala la maadili na uwajibikaji yanayozigusa Wakala za Serikali.
Aliainisha masuala hayo ni pamoja na watumishi hewa, taarifa chafu za
watumishi, matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za umma,
kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa mifumo ya utendaji kazi na wakati
mwingine kutotekeleza majukumu ya msingi ya wakala.
Alifafanua kuwa amegundua kupitia taarifa mbalimbali kuwepo kwa
changamoto ya mawasiliano hafifu kati ya wizara mama na wakala zilizo
chini yao ambapo taarifa kutoka katika wakala hazichambuliwi
inavyostahili na hata zinapochambuliwa na wizara mama, hazitoa mrejesho
kwenda katika wakala.
Awali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Utumishi), Dk Laurean Ndumbaro
alizitaka wakala za serikali kuimarisha eneo la ufuatiliaji na tathmini
ili kuimarisha utendaji kazi na kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na
Watanzania
Monday
RELATED STORIES
Rais Magufuli amsimamisha kazi Kaimu Katibu wa Tume ya MipangoRais John Magufuli amemsimamisha kazi Kaimu Katibu wa Tume ya Mipango (Wizara ya Fedha), Florence
Fahamu unywaji pombe salama unaoweza kuimarisha afya yakoKipimo salama na sahihi kwa afya bora cha unywaji wa pombe kinabadilika kutokana na umri. Ongea na
Jeshi la Polisi Dar layataja matukio makubwa ya mwaka 2016Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imekamata jumla ya watuhumiwa 13,626 na kuwafikish
Vita ya dawa za kulevya: 12 kati ya 112 kupandishwa kortini akiwemo Wema, TID na wengineSakata la Madawa ya kulevya limeendelea kugonga vichwa vya habari wiki hii ambapo Jumatatu hii Jes
Hili ni ombi la Rais Magufuli kwa Watanzania mwaka 2017Rais wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaomba Watanzania wote kuutunza na kuudumisha umoja k
Ifaham Gharama ya kuilinda familia ya Trump kwa siku Familia ya Rais wa Marekani, Donald Trump ina ulinzi mkali. Ulinzi huo unadaiwa kugharimu kiasi kik
0 maoni: