Ni kwasababu simu za kizamani, hazitoweza kukubali mabadiliko yatakayoongezeka kwenye app hiyo. WhatsApp imetoa tangazo hilo wakati ikisherehekea kutimiza miaka 7 tangu ianze kufanya kazi mwaka 2009.
App hiyo kwa sasa inatumiwa na watu zaidi ya bilioni 1 duniani.
Kupitia blog yake, WhatsApp imetaja simu itakazoziacha kuwa ni pamoja na zinazotumia mfumo wa Android 2.1 na Android 2.2; Windows Phone 7 na iPhone 3GS/iOS 6. Na hadi June 2017, WhatApp haitopatikana kwenye BlackBerry 10; Nokia S40; na Nokia Symbian S60.
0 maoni: