MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji La Arusha, Athumani Kihamia ametangaza
kusitisha mikataba ya wafanyakazi 66 kati ya 132 wasio na kazi za
lazima katika halmashauri hiyo.
Amewasimamisha kazi kwa lengo la kubana matumizi ili fedha
zitakazookolewa zitaelekezwa kwenye matumizi ya miradi ya maendeleo na
ulipaji wa madeni.
Alisema hayo wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake, na kueleza
kuwa kabla ya hapo, alikuwa akilipa mishahara ambayo aliibebesha
halmashauri mzigo huo mkubwa na kufanya ielemewe na kupoteza fedha
ambazo zingetumika kwenye miradi ya maendeleo na ulipaji wa madeni.
Kihamia alisema anasimamia kubana matumizi ili kulipa madeni yenye kero
na tija kama ambavyo walielekezwa na Kamati za Bunge na Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhakikisha wanabana matumizi
yasiyo na ulazima ili kulipa madeni ya muda mrefu.
Akizungumzia tuhuma za ulipaji wa fedha za walimu 701 kiasi cha Sh
milioni 169 zikiwa madeni ya walimu ambazo hazikufuata utaratibu wa
kuidhinishwa na Baraza la Madiwani au Kamati ya Fedha na Uchumi, alisema
fedha hizo zinatokana na mapato ya ndani nasi lazima fedha zinazotumika
kuidhinishwa na baraza au kamati ya fedha.
Thursday
RELATED STORIES
Rais Magufuli mbioni kuhamia DodomaRais wa Jamhuri wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametembelea uwanja wa Chamwino mkoani Dodoma n
Ndege ya kijeshi yenye watu 90 yapotea kwenye radarNdege ya kijeshi ya Urusi imepotea kwenye radar dakika chache tu baada ya kupaa angani kutoka kweny
Taarifa rasmi kutoka Clouds Media kuhusu video inayosambaa
Rais Magufuli amsimamisha kazi Kaimu Katibu wa Tume ya MipangoRais John Magufuli amemsimamisha kazi Kaimu Katibu wa Tume ya Mipango (Wizara ya Fedha), Florence
MTUMISHI ASIEWASILISHA CHETI CHAKE IFIKAPO MACHI MOSI MWAKA HUU KAJIFUKUZISHA KAZI MTUMISHI wa umma atakayeshindwa kuwasilisha cheti cha elimu na taaluma au “Index number” ya mtih
Spika ana mamlaka kisheria ya kuomba vyombo vya dola kumsaidia kumkamata mtu – MdeeMbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amesema Spika ana mamlaka ya kisheria ya kuomba vyombo vingi
0 maoni: