Saturday

Jeshi la Polisi Dar layataja matukio makubwa ya mwaka 2016

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imekamata jumla ya watuhumiwa 13,626 na kuwafikishwa mahakamani kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo dawa za kulevya na ujambazi wa kutumia silaha kwa kipindi cha mwaka mmoja wa 2016.
Hayo yamehainishwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro. Amesema oparesheni zilizofanyika kwa kutumia vikosi mbalimbali vya Jeshi hilo vikiwemo vikosi maalum cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha,kikosi cha Kuzuia wezi wa magari,Kikosi cha Mbwa na Farasi, Kikosi cha Askari Kanzu,kikosi maalum cha kukamata wezi wa mifugo, kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya na Kikosi cha Kuzuia ghasia( FFU) zimeweza kuleta mafanikio mbalimbali.
“Idadi ya watuhumiwa 7625 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kupatikana na bangi kilogramu 2843 na gramu 78. Jumla ya watuhumiwa 269 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya madawa ya kulevya ya aina mbalimbali kama Cocaine kilo 3 gramu 255,Heroinekilo 1 gramu 654,” alieleza Kamanda Sirro.
Kamanda huyo aliendelea kutaja matukio hayo ikiwa ni pamoja na pombe haramu ya Gongo jumla ya lita 8547, mitambo 34 na watuhumiwa wapatao 5627 kwa mwaka mzima walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
“Watuhumiwa 126 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya Madawa ya kulevya aina ya Mirungi kilo 75 na gramu 254. Jumla ya Silaha 67 na risasi 1076 za aina mbalimbali zilikamatwa pamoja na watuhumiwa 52 na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha. Jumla ya wahamiaji haramu 105 toka mataifa mbalimbali walikamatwa na kufikishwa mahakamani.”
Kamanda huyo aliongeza kuwa hali ya uhalifu wa kutumia silaha katika jiji la Dar es Salaam umepungua, ukilinganisha na mwaka uliopita wa 2015 na matukio yaliyoongezeka kwa wingi ni ya ubakaji na ulawiti.

SHARE THIS

0 maoni: