Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma
Watumishi
wa Umma 1,663 kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali,
Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa wamechukuliwa
hatua za kinidhamu baada ya kubainika kusababisha watumishi hewa 19,629
hadi Oktoba 25, 2016.
Waziri
ya Nchi, Ofisi ya Rais, anayeshughulikia Utumishi na Utawala Bora
Angella Kairuki amesema hayo jana Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu
swali la Mainda Hamad Abdallah (Mbunge wa Viti Maalum) alilohoji hatua
zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya watumishi waonarudisha nyuma
maendeleo ya nchi.
Akifafanua
idadi hiyo, Waziri Kairuki alisema kuwa idadi ya watumishi
waliochukuliwa hatua za kinidhamu kutoka Wizara mbalimbali ni 16, Idara
zinazijitegemea na Wakala za Serikali watumishi tisa, Sekretarieti za
Mikoa watumishi sita na Mamlaka za Serikali za Mitaa watumishi 1,632.
Waziri
Kairuki alisema kuwa watumishi hao wameisabishia Serikali hasara ya
zaidi ya Sh. bilioni 19, huku Halmashauri ya Kinondoni ikiwa na
watumishi hewa 107 ambao waligharimu Serikali sh. bilioni 1.29, Kishapu
watumishi 73 wamesababisha hasara ya kwa kugharimu sh. milioni 543 na
kuonya kuwa waajiri waendelee kuchukua hatua za haraka na kudhibiti
uwepo wa watumishi hewa ili kuipunguzia Serikali kuingia hasara kubwa
badala ya kuwahudumia wananchi.
Aidha,
Waziri Kairuki alisema kuwa jumla ya watumishi 638 wamefunguliwa
mashtaka polisi, watumishi 50 wanafanyiwa uchunguzi na Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na watumishi 975 mashtaka yao
yamefikishwa kwenye Mamlaka zao za kinidhamu.
0 maoni: