Katika kipindi cha kuanzia march 22 2016
hadi June 30 2016 Serikali ilifanya zoezi la uhakiki wa silaha zote za
kiraia Tanzania bara. Baada ya zoezi hilo kukamilika Makao makuu ya
Jeshi la polisi wametoa tathmini ambapo imeonyesha kuwa asilimia 59.18
tu ya silaha zote zilizosajiliwa ndiyo zilihakikiwa wakati 40.82
hazijahakikiwa kwa sababu wamiliki hawakujitokeza kuzihakiki..
Leo November 18 2016 makao makuu ya jeshi la polisi kupitia kwa kaimu mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai, Robert Boaz
amesema kuwa kwa sababu wanatambua huenda zipo sababu za msingi kwa
baadhi ya wamiliki kushindwa kujitokeza hivyo wamewataka wamiliki ambao
hawajahakiki silaha zao kuhakiki silaha zao ndani ya kipindi cha mwezi
mmoja kuanzia November 11 hadi December 20 2016 na utakapomalizika
watachukua hatua kali.
0 maoni: