Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa imesema tatizo la rushwa bado
ni kubwa nchini kutokana wanaojihusisha na vitendo hivyo kubuni mbinu
mpya za kisasa za kufanikisha mipango hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kupambana na
Kuzuia Rushwa, Valentino Mlowola, Jumanne hii wakati wa kongamano la
wanafunzi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya siku ya maadili na Haki za Binadamu. “Sheria ya rushwa na mapambano yamekuwa yanaendelea yanabadilika kadri ya muda unavyokwenda. Leo hivi sasa tulikuwa na miaka hivi ya 70 kulikuwa na kikosi cha kupambana na rushwa tulikuwa tunaandaa hii mitego mitego, tunaenda kukaa mahali kuangalia watu wanaopokea rushwa tunawakamata. Lakini angalia changamoto za sasa hela inakwenda kwa tigo pesa lazima tubadilishe mbinu, social problem yoyote haiwezi kuwa kirahisi namna hiyo,” amesema Mlowola.
Hivi karibuni Rais Dkt John Magufuli akiwa ikulu na wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa vyombo mbalimbali nchini alisema kuwa rushwa ni kansa ya maendeleo ya nchi na kumuomba kila mwananchi kuikwepa.
0 maoni: