Serikali imewataka walimu kuwapa adhabu wanafunzi kulingana na mwongozo
uliotolewa na serikali katika waraka wa adhabu wa mwaka 2002 huku
akiwaasa wazazi kutowatetea watoto wao pindi wanapokosa nidhamu
mashuleni.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako, alisema hayo Jumanne hii alipofungua mjadala wa wanafunzi
kuelekea maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu, uliofanyika jijini
Dar es Salaam.Waziri Ndalichako amesema kuwa wazazi wamekuwa wakiwavunja nguvu walimu kwa kuwatetea watoto wao hata kama wamekosa hivyo wanapaswa kuwa makini katika hili.
“Sasa hivi tumekuwa na changamoto ambazo unakuta wazazi wengine wanapenda kutetea watoto wao pindi wanapokuwa wanajiingiza katika utovu wa nidhamu,sasa hali kama hiyo inakuwa inawavunja nguvu walimu kwasababu unakuta bodi za shule hazifanyi kazi zao vizuri wazazi wanakuwa zaidi upande wa watoto wao kuwatetea hata pale ambapo inapaswa kukemea,” alisema Ndalichako.
Aidha waziri huyo ameendelea kuwasihi wazazi kushirikiana kwa karibu na walimu watoto wanapokuwa wakipewa adhabu na kuacha tabia ya kurudi upande wa watoto wao na kuwatetea.
0 maoni: