Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza ziara yake katika
wilaya Kinondoni ambapo asubuhi ya leo amezungumza watumishi wa wilaya
hiyo pamoja na kutoa baadhi ya maagizo.
Akiongea na watumishi wa wilaya hiyo, Makonda amewataka watumishi
kufanya kazi kwa bidii huku akidai kuna baadhi ya watumishi wanashinda
kwa waganga wakienyeji ili wasitumbuliwe.
“Kuna baadhi ya watumishi wanatembea na hirizi ili wasitumbuliwe,
wakikutana na viongozi wao wanazibinya,” alisema Makonda. “Mimi
ninachokitaka kutoka kwenu ni kuwatumikia wananchi wa chini,”
Pia Makonda amewataka wakuu wa wilaya wote kuanzisha kitengo maalum
cha kisheria kitakacho tumika kutoa elimu kuhusu migogoro ya ardhi na
kuwashauri wananchi kabla ya kupeleka malalamiko yao mahakamani na
kuwaweka wazi kama kuna dalili ya kushinda au vinginevyo na kuwapa
suluhisho la kudumu.
Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka DC Hapi na Meya wa
Kinondoni Bernard Sita kufuatilia suala la vibali vya ujenzi na
kuhakikisha vinatoka kwa wakati ili kuharakisha maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Hapi amehaidi
kuwashughukia watendaji wote watakao bainika kutowajibika kikamilifu ili
kuchochea maendeleo.
0 maoni: