Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ametoa
mwezi mmoja kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi za kijiji hadi mkoa
kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo yao.
Lukuvi ametoa agizo hilo alipokutana na viongozi wa ngazi mbalimbali
katika mkoa wa Kigoma ambapo amesema mazoea ya kugawa maeneo bila
kuzingatia vigezo ndiyo yamesababisha kuwepo kwa migogoro kila maeneo
nchini na sasa ni jukumu la waliogawa kufanya kazi ya kuitatua katika
kipindi cha mwezi mmoja.
“Viongozi wote wa mikoa na wakuu wa wilaya jukumu la kutatua migororo
ya vijiji ni lenu kwasababu nyinyi ndiyo mliopendekeza vijiji vigawiwe,
nyinyi ndio mliopendekeza kata zigawiwe na nyinyi ndiyo mliopendekeza
vijiji na kata. Kwahiyo nendeni chini kule mkatatue na ningefurahi nchi
nzima hii ifikapo tarehe 30 mwezi Disemba muende kwenye maeneo yote
kwenye orodha yote mliyoisema ya migogoro ya vijiji mkatatue kwa
kushirikiana na wale wananchi,” alisema Lukuvi.
Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam katika ziara yake ya siku
10 jijini Dar es salaam amekuwa akikumbana na migogoro mingi ya ardhi
katika mkoa wake.
0 maoni: