Showing posts with label VIDEOS. Show all posts
Showing posts with label VIDEOS. Show all posts

Sunday

Saturday

Wednesday

SAIDA KALORI ADAI MENEJA WAKE ALIMTAPELI DIAMOND YEYE HAKUPATA HATA MIA

SAIDA KALORI ADAI MENEJA WAKE ALIMTAPELI DIAMOND YEYE HAKUPATA HATA MIA


Msanii wa zamani wa muziki wa asili Saida Karoli amedai yeye anasikia kama watu wengine kwenye vyombo vya habari kwamba Diamond ameiangia mkataba na meneja wake wa zamani kuhusu kutumia vionjo vya nyimbo zake katika kutengeneza wimbo ‘Salome’ wa Diamond.
Muimbaji huyo amedai hizo asilimia 25 za mapato za wimbo ‘Salome’ ambazo zilielezwa na viongozi wa WCB hazijui kwa kuwa hakuhusishwa kwenye hilo.
“Tatizo limekuja kwa meneja wangu aliyempatia Diamond kazi, mimi nimempatia bure Diamond hiyo kazi aitumie,” alisema Saida katika runinga ya KUTV ya nchini Kenya. “Lakini kwenye kusikia masikioni kwangu na kwenye vyombo vya habari kwamba Diamond amempatia pesa milioni 25 meneja wangu wakawa wametengeneza mkataba kwamba huu wimbo utatumika hivi na hivi ila mimi kama mimi huo mkataba siujui na wala sikuuona na wala hawakunionyesha. Mimi ninachojua nimempatia kazi Diamond bure ili aitumie tuinuane wasanii wa Tanzania,”
Pia muimbaji huyo amedai yeye alishiriki kiasi fulani katika kuandaa kiitikio cha wimbo huo kwa kuingiza sauti yake.
Diamond na uongozi wake baada ya kuachia wimbo huo, walionyesha picha wakati wakifanya makubaliano na meneja wa zamani wa Saida.
“Kitu tulichokifanya kabla ya kurelease wimbo, tulizungumza na uongozi wake, tukawaambia tunafanya hiki na hiki na kuna kiasi pia tukakitoa ili kiende kwake halafu tukampa 25% ya publishing. Kila income ya publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa anapata percent,” Diamond alikiambia kipindi cha 255 cha Clouds FM.

Monday

Muonekano wa ndani wa ndege binafsi ya Donald Trump

Muonekano wa ndani wa ndege binafsi ya Donald Trump


Rais mteule wa Marekani Donald Trump ni miongoni mwa watu matajiri nchini Marekani. Bilionea huyu ni mfanyabaishara anayemimiliki mashamba na hoteli mbalimbali nchini humo. Katika wakati wote wa kampeni, Donald Trump alikuwa akitumia ndege yake binafsi katika safari zake.
Kwa vile sasa amechaguliwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani atalazimika kuiacha ndege hiyo na kutumia ndege maalum ya Rais ‘Air Force One’ ambayo ndiyo hutumiwa na rais wa nchi hiyo.

 Hapa chini ni video ikikuonyesha muonekano wa ndani wa ndege binafsi ya Donald Trump.

Saturday

Friday

 Maandamano ya kumpinga Donald Trump yaingia siku ya pili

Maandamano ya kumpinga Donald Trump yaingia siku ya pili

Maelfu ya watu wanaopinga ushindi wa Donald Trump kwenye uchaguzi wa Urais, wameendelea kuandamana mtaani kwa usiku wa pili sasa katika miji mbalimbali nchini Marekani.
Waandamanaji wa huko Portland, Oregon, walikabiliana vikali na polisi. Kile kilichoanza kama maandamano ya amani ya watu zaidi ya 4,000, kimegeuka kuwa na fujo.
Watu hao wameharibu biashara, magari na kuwatupia vitu polisi. Maandamano mengine yanaendelea kwenye miji ya Los Angeles, Philadelphia, Denver, Minneapolis, Baltimore, Dallas na Oakland, California.
Rais huyo mteule, Trump ameyalaani maadamano hayo.


Sunday

Wednesday