Sunday

Q Boy Msafi akana kuupinga mtandao wa wasafi.com

Msanii wa Bongo Fleva, Q Boy Msafi ambaye alikuwa mbunifu wa mavazi ya Diamond Platnumz amesema si kweli alikuwa anapinga ujio wa mtandao wa wasafi.com kitu kilichopelekea kutimuliwa WCB.

Q Boy ameiambia kipindi cha cha The Play List cha Times FM,  wakati mtandao huo unaanzishwa yeye tayari alikuwa nje ya WCB.
“Suala la wasafi.com hata walipozindua mimi sikuwepo. Hata maandalizi for real nilikuwa mbali na vikao ambavyo walikuwa wanafanya kwa sababu nilikuwa out of wasafi na nilikuwa nimeshanza kufuatilia ishu zangu lakini nilikuwa na fununu kuwa wasafi wanafungua mtandao,” amesema Q Boy.
Katika hatua nyingine Q Boy amesema sababu ya wimbo wake mpya ‘Karorero’ kutokuwepo katika mtandao huo ni kwamba tayari alikuwa ameshauuza kwa watu wengine.
“Wimbo wangu wa pili sikuupeleka ila bosi Tale aliniandikia kwenye Whats App fanya ulete wimbo wako kwenye wasafi .com lakini mimi nilikuwa nimeshakaa chini na watu ambao nilitaka kuwapa caller tunes, so sikuweza kuchanganya,” ameongeza.

SHARE THIS

0 maoni: