Sunday

 Mbwana Samatta aipatia Taifa Stars ushindi wa mabao 2-0

Mbwana Samatta aipatia Taifa Stars ushindi wa mabao 2-0

Mbwana Samatta amefanya kile ambacho watanzania wengi walikuwa wanatarajia akifanye, magoli mawili aliyofunga yameipa Stars ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa ya kalenda ya FIFA iliyochezwa kwenye uwanja wa taifa.
Samatta alianza kuweka kambani dakika ya pili tu tangu kuanza kwa kipindi cha kwanza baada ya kutoka na mpira nje ya box na kuwakusanya mabeki wa Botswana na kuingia nao kwenye box kisha kumtungua kwa mguu wa kushoto golikipa wa Botswana ambaye aliruka bila mafanikio.
Bao hilo lilidumu kwa dakika zote zilizobaki za kipindi cha kwanza huku mchezo ukiwa umechangamka kwa timu zote kushambuliana kwa zamu.
Kipindi cha pili Botswana waliamua kuliandama goli la Stars kwa mashambulizi ya mara kwa mara kwenye goli la Stars na mara kadhaa walipoteza nafasi za kufunga.
Dakika ya 87 kipindi cha pili, Samatta alifunga goli la pili na la ushindi kwa Stars kwa mkwaju wa free-kick nje kidogo ya box la penati baada ya yeye mwenyewe (Samatta) kuangushwa nje kidogo ya eneo la penati box.
Licha ya kufunga magoli mawili, Samatta aliwa kwenye wakati mgumu kwa sababu mara nyingi alikuwa akichezewa rafu zilizosababisha wachezaji wa Botswana kuoneshwa kadi za njano. Samatta ilibidi atibiwe na daktari wa Stars baada ya kufanyiwa rafu wakati akijaribu kumtoka moja ya mabeki wa Botswana.
Umahiri wa golikipa wa Botswana Kabelo Dambe umeisaidia timu yake kupunguza idadi ya magoli kutokana na kuokoa michomo ya miwili ya Mbwana Samatta pamoja na Simon Msuva.
Taifa Stars itacheza tena mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi siku ya Jumanne March 28, 2017 kwenye uwanja wa taifa.
 Nay wa Mitego kukamatwa na polisi ni kutokana na wimbo wake Wapo

Nay wa Mitego kukamatwa na polisi ni kutokana na wimbo wake Wapo

Nay wa Mitego amedai amekamatwa na polisi wilayani Mvomero, Morogoro alikokuwa ameenda kwaajili ya show.
Hajasema sababu ya kukamatwa kwake lakini watu wanahisi ni kutokana na wimbo wake Wapo ambao umemkosoa vikali Rais Dkt John Magufuli. “Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police,” ameandika rapper huyo mtata.
“Nawapenda Watanzania wote. #Truth #Wapo,” ameongeza.
 Mbwana Samatta anamiliki mijengo sita Dar

Mbwana Samatta anamiliki mijengo sita Dar

Achana na uwezo wa Mbwana Samatta akiwa uwanjani. Mchezaji huyo siyo wa mchezo pia kiuchumi– ana mijengo takribani sita jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti, mshambuliaji huyo wa Taifa Stars na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amewekeza zaidi katika kujenga nyumba ambazo zote hizo zipo Mbagala lakini katika maeneo tofauti tofauti.
Imedaiwa kuwa mijengo hiyo ya Samatta ipo Majimatitu, Kiburugwa Shimo la Mchanga, Mbande na Mbagala Saku (zote zipo Mbagala) ukiachana na ile ikulu yake anayoijenga huko kibada ambayo tayari imeisha japo kuna marekebisho madogo madogo yanaendelea.
Wakati huo huo rafiki wa karibu wa mchezaji huyo aliliambia gazeti hilo kuwa mchechezaji huyo anaishi katika nyumba yake aliyopanga (Apartment) iliyopo katika ufukwe wa bahari ya Hindi maeneo ya Kijichi.
“Anapokuja kwa mapumziko kwao huwa anakwenda kwa sababu ni nyumbani kwa ajili ya kusalimia na mambo mengine lakini hakai hapo, anaishi Kijichi kuna nyumba nzuri ya kifahari ipo ufukweni mwa bahari amepanga,”alisema.

Monday

Taarifa rasmi kutoka Clouds Media kuhusu video inayosambaa

Taarifa rasmi kutoka Clouds Media kuhusu video inayosambaa

Kufuatia kusambaa kwa video mitandaoni ikiaminika ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiingia Clouds Media akiwa na askari, Uongozi wa Clouds Media Group umetoa taarifa rasmi leo March 19 2017.
Taarifa imesema…>>>’Kumekuwa na habari mbalimbali kuhusu Clouds Media Group na viongozi mbalimbali akiwemo Askofu Josephat Gwajima na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda. Kiini cha habari zote hizo ni uwepo wa taarifa zinazomhusu mwanamke anayedai kuzaa na Askofu Gwajima
Ni kweli habari ya uwepo wa mama huyo ilitufikia kupitia kipindi chetu cha De Weekend Chat Show (SHILAWADU) lakini baada ya uchunguzi wa kina tuligundua kwamba habari haina mashiko, inakosa vigezo vya habari inayofaa kuonyeshwa na hivyo tulisimama katika kanuni za taaluma yetu na kuzuia kabisa kuonyeshwa kwa taarifa hiyo
Kizuizi hicho kilifuatiwa na matukio mbalimbali ikiwemo mijadala inayosambaa juu ya Mkuu wa mkoa Paul Makonda kuvamia ofisizetu. Jambo hilo limezua hofu na taharuki kubwa kwa wadau wote pamoja na kusababisha mashaka miongoni mwa wafanyakazi na viongozi wa Clouds Media Group
Pamoja na yote jambo hili lipo katika uchunguzi wa kina unaofanywa na sisi Clouds Media Group kwa kushirikiana na mamlaka zote husika, tunaomba wapenzi, wadau na Watanzania wote wawe na subira wakati tunajiandaa kutoa tamko rasmi kuhusu yaliyotokea
.
Ifaham Gharama ya kuilinda familia ya Trump kwa siku

Ifaham Gharama ya kuilinda familia ya Trump kwa siku

Familia ya Rais wa Marekani, Donald Trump ina ulinzi mkali. Ulinzi huo unadaiwa kugharimu kiasi kikubwa cha fedha.
Wakati ambapo Trump alihamia kwenye ikulu ya White House iliyopo jijini Washington DC, mke wake Melanie, na mwanae wa mwisho, Barron bado wanaishi New York.
Muda mfupi baada ya uchaguzi, ripoti ya CNN Money ilionesha kuwa kuilinda familia ya Trump mjini New York hugharimu dola milioni 1 kwa siku.
Kama wakiamua kuungana na Trump White House, gharama hiyo itapungua kwa kiasi kikubwa.
Hilo si jambo pekee linalozungumzwa kwa sasa. Tangu mwaka uanze, Trump ameenda mapumzikoni mara nne huko Mar-a-Lago Florida. Kwa mujibu wa wachambuzi wa gazeti la Politico, safari hiyo hugharimu dola milioni 3 kila akienda.
Diamond afungua mwaka na deal hii kubwa ya ubalozi

Diamond afungua mwaka na deal hii kubwa ya ubalozi

Msanii wa muziki Nassib Abdul maarufu, Diamond Platnumz ameteuliwa rasmi na kampuni ya GSM kuwa balozi wa kutangaza bidhaa mbalimbali za taasisi hiyo.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Afisa Masoko wa kampuni hiyo, Lauma Mohamed ameeleza kuwa Diamond
Platnumz ni msanii mkubwa sana ndani na nje ya Afrika, hivyo wanaimani atakuwa balozi mzuri kwa bidhaa zao
bora kwa watanzania.
Kwa upande wake Diamond Platnumz ameeleza kuwa anafarijika sana kuona wasanii watanzania wanapata nafasi
ya kuwa mabalozi, kwani wasanii ni wengi lakini yeye amepata heshima hiyo hivyo ana imani ni jambo jema kwa tasnia ya muziki.
Ameongeza kuwa hapo mwanzo bidhaa nyingi kwa mfano samani za ndani zilikuwa zinaagizwa nje ya nchi lakini kwa
sasa itakuwa rahisi kwani GSM kwenye duaka lao la ‘The New Home’ wanauza samani hizo halkadhalika nguo za watoto.
Licha ya kumtambulisha msanii huyo kama balozi mpya wa GSM wamezindua matangazo mapya mawili yaliyoigizwa na msanii
huyo pamoja na familia yake akiwemo Zari the Boss Lady na mtoto wao Tiffa, huku tangazo moja likiwa la nguo na lingine la samani za ndani.

Friday

Rais Magufuli mbioni kuhamia Dodoma

Rais Magufuli mbioni kuhamia Dodoma

Rais wa Jamhuri wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametembelea uwanja wa Chamwino mkoani Dodoma na kuwahakikishia wananchi kuwa atahamia Dodoma hivi karibuni kama alivyoahidi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga kuhusu kazi za ufyatuaji wa Matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Ikulu Chamwino mkoani Dodoma
Hii ni taarifa yake: